Kwa mujibu wa shirika la habari la Ahlul Bayt (as) -ABNA- Mohammed al-Bukhaiti, Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah, katika mahojiano na televisheni ya Al-Mayadeen, alitangaza kuwa shambulio dhidi ya kikao cha Serikali ya Yemen huko Sana'a ni kuvuka mistari miekundu, na kwamba vita imeingia katika awamu mpya.
Alisisitiza kuwa: "Kisasi ni hakika, na matendo yetu yatatangulia maneno yetu."
Katika kuendeleza mahojiano hayo, al-Bukhaiti alieleza kuwa suala la Palestina ni "kipaumbele cha kwanza" kwa harakati ya Ansarullah, na akaongeza kuwa kauli za hivi karibuni za rais wa Yemen, Mahdi al-Mashat, zimethibitisha tena msimamo thabiti wa harakati hiyo wa kuiunga mkono Palestina na Gaza.
Akinukuu mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel, alieleza kuwa: "Wavamizi hawawezi kuvunja dhamira ya watu wa Yemen, na Ansarullah itaendelea kuiunga mkono Gaza kwa gharama yoyote ile."
Al-Bukhaiti pia alibainisha kuwa Yemen iko katika hali ya vita, na hadi sasa imewasababishia maadui mashambulizi kadhaa.
Akaongeza: "Kupokea mashambulizi ni jambo linalotegemewa," lakini alisisitiza kuwa Ansarullah imefanikiwa kuwaadhibu Uingereza na Marekani, na itaendeleza njia hiyo hiyo dhidi ya adui wa Kizayuni (Israel).
Inapaswa kusemwa kwamba, kwa mujibu wa taarifa ya urais wa Yemen huko Sana'a, katika shambulio la siku ya Alhamisi, Waziri Mkuu wa Yemen, Ahmad Ghalib al-Rahwi, pamoja na mawaziri kadhaa waliuawa shahidi, huku wengine wakijeruhiwa vibaya.
Your Comment